SUA Family inayofuraha kubwa kukukaribisha tena kwenye jukwaa lako. Hapa utapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wataalam wa kada mbali mbali waliosoma katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine Morogoro Tanzania (SUA) pamoja na watalaam wengine wenye utalaam wa fani mbali mbali nje ya kilimo waliopata ujuzi wao vyuo vingine zaidi ya SUA.
Unakaribishwa kutoa mchngo wako wa mawazo kwa kuandika makala au kutoa maoni au hata kutuma picha katika blog hii kwa ajili ya kuongeza tija katika utendaji wetu wa kulitumikia taifa letu la Tanzania.
Blog hii inatumika kama nyenzo ya kuchangisha mawazo chanya na pia kama sehemu ya miundo mbinu ya kufikisha mawazo mahali yanapotakiwa.
Ni matumaini yetu utapata nafasi ya kupanua wigo wa uwajibikaji na kuleta matokeo chanya kwa kujisikia ni sehemu ya familia yetu kwa kukaa nasi hapa siku ya leo na kesho pia.